Nilipokea wimbo huu wiki kadhaa zilizopita. Majukumu yakawa mengi.Unga ukazidi maji. Na kwa sababu nilishaona wimbo ni kutoka kwa some of the finest young Hip Hop artists wa Tanzania nikaona ngoja nitulie nikipata wakti nitausikiliza kwa makini na kisha kuuweka hapa. Sikukosea na sijutii.
Kama kawaida, ni wimbo wenye maudhui mengi.Lakini ukimaliza kuusikiliza unataka kumwambia mwenzio. Naam,unaitwa Mwambie Mwenzio. Ni kutoka kwa Stamina, Darasa na Warda. Tiddy Hotter ndio mpishi.
*TRACK NAME: Mwambie Mwenzio
ARTIST NAME: Stamina Ft Darasa & Warda
COMPOSED BY Stamina
PRODUCER: TIDDY HOTTER
STUDIO: ONE LOVE FX