Katika maandiko matakatifu ya dini ya kikristo yaani Biblia, mke mwema ameongelewa vizuri katika Mithali 31. Pale “Mke Mwema” ameelezewa aweje na vitu gani vinaweza kumtambulisha.
Ukweli ni kwamba tunaishi katika dunia tofauti. Zama walizoishi babu zetu tumeshazipoteza. Tumepoteza mila na hata miiko. Bahati nzuri ni kwamba hatujafika. Bado tupo safarini. Yawezekana kumpata “Mke Mwema”.
Nimeikumbuka mistari ya Mithali 31 niliposikiliza wimbo mpya kutoka kwa Black Rhino akimshirikisha Soprano ambao umepewa jina Mke Mwema. Pengine haina uhusiano lakini kwa sababu moja au nyingine nimekumbuka Mke Mwema.
On a side note: Huu naamini ni mojawapo ya nyimbo nzuri zaidi kutoka kwa Black Rhino ambaye mwaka jana alifunga ndoa na mpenzi wake wa siku nyingi, Beatrice. Well done Rhino. Usikilize hapa.